Historia yetu
Kujua historia ya dayosisi yetu ya Dar es salaam
Kanzi data
Kupata huduma mbalimbali kwa njia ya kieletroniki
Sinodi
Kupata taarifa mbalimbali za sinodi iliyopita
Karibu Kanisa Anglikana, Dayosisi ya Dar-es-salaam
“Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.”
Zaburi 119:105
Tukiwa tumejikita mizizi katika imani na huduma za kiroho na kijamii, Kanisa Anglikana dayosisi ya Dar es Salaam ni jumuiya ya Kikristo inayolenga kumtangaza Kristo, kukuza imani ya waumini, na kubadilisha maisha ya jamii yetu kwa ujumla kwa kuzingatia misingi ya upendo na huruma.
Kupitia ibada zetu, na huduma za kijamii kama elimu, afya, na huduma nyinginezo za kijamii, dayosisi yetu inalenga kumtukuza Mungu na kuwahudumia watu wake kwa uaminifu na moyo wa upendo.
Ujumbe kutoka kwa Askofu
✝️Ni sisi Jackson
Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam
Kuhusu Dayosisi
“Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.”
Mathayo 5:16
Kanisa Anglikana dayosisi ya Dar es Salaam ni mojawapo ya dayosisi muhimu ndani ya Kanisa Anglikana Tanzania. Ina mitaa na vigango yenye uhai vilivyomo ndani ya achidikonari tisa, ambazo ni Ubungo, Kinondoni, Ilala, Temeke, Kibaha, Upanga, Bagamoyo, Ukonga na Kigamboni. Makanisa haya yanayoongozwa na wachungaji, mashemasi,wainjilisti, na viongozi mbalimbali ambao ni sehemu ya waumini.
Idara Zetu
Kanisa Anglikana dayosisi ya Dar es Salaam inatoa huduma mbalimbali ambazo zinatolewa na idara zilizoko chini ya ofisi ya katibu na idara zilizoko chini ya ofisi ya kasisi mkuu. Idara zetu zimegawanyika katika makundi makuu 3, Idara za kiutawala ambazo zinasimamia shughuli za kila siku za utawala, zipo idara ambazo ni taasisi zinazotoa huduma za kijamii, na kuna idara ambazo zinaundwa na waumini waliojiweka kwenye makundi tofauti ya rika na jinsia.
Takwimu za Dayosisi
Pata taarifa fupi kuhusu dayosisi yetu kwa kupitia takwimu hizi
Habari na Matukio
“Njoni tumwabudu, tupige magoti mbele za Bwana Mtengenezaji wetu.”
Zaburi 95:6
Pata taarifa za matukio mbalimbali yanayotokea ndani ya dayosisi, ikiwemo ibada kwenye mitaa na vigango mbalimbali, ziara mbalimbali za Askofu, ziara za kichungaji, na huduma za jamii kupitia chanel yetu ya Anglican Tv.
ili kufuatilia vipindi na ibada mbalimbali tafadhali bofya kitufe hapo chini
Ibada zetu
Ilipo Mitaa yetu
Ungana nasi kila Jumapili kwenye ibada kwa lugha ya Kiingereza kwenye baadhi ya mitaa yetu na ibada kwa lugha ya Kiswahili katika mitaa,na vigango vyetu vyote.
Pia tuna ibada za katikati ya juma, pamoja na ibada za jumuiya kila siku ya jumamosi, kwenye mitaa na vigango husika.
Wasiliana nasi
Kupata huduma , taarifa na msaada wa kiroho na kiutendaji kutoka dayosisi tafadhali wasiliana nasi au tutembelee ofisini
Nyumba no. 35
Mtaa wa Arusha/Moshi
Ilala, Dar es salaam
+255 745 960 998
+255 760 960 883
+255 716 959 995
info@anglicandar.org
actdiosm@gmail.com
habari@anglicandar.org
- Today's visitors:7
- Today's page views 7
- Total visitors 261
- Total page views 273


