Usajili wa Mitaa
Kanisa Anglikana dayosisi ya Dar es salaam, ina jumla ya mitaa 94 iliyoko chini ya Archidikonari 9. Dhumuni la kusajili mitaa hii ni ili kuweka kumbukumbu za mitaa, maeneo iliko, pamoja na rasilimali zinazomilikiwa na dayosisi chini ya mitaa hiyo. Taarifa hizi zitawezesha dayosisi kufanya maamuzi sahihi ya mgawanyo na utunzaji wa rasirimali, watu na vitu, lakini pia zitasaidia kwenye kupanua wigo wetu wa kueneza injili kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa bado.
Fomu hii ni mahususi kwaajili ya kusajili mitaa yote iliyoko chini ya kanisa Anglikana, dayosisi ya Dar es salaam, fomu hii ijazwe na Kasisi/ Katibu wa mtaa/ kiongozi wa mtaa aliyeidhinishwa na mtaa kusimamia maswala ya kiutawala ya mtaa husika.
Jaza fomu hii
Wasiliana nasi
Kupata huduma , taarifa na msaada wa kiroho na kiutendaji kutoka dayosisi tafadhali wasiliana nasi au tutembelee ofisini
Nyumba no. 35
Mtaa wa Arusha/Moshi
Ilala, Dar es salaam
+255 745 960 998
+255 760 960 883
+255 716 959 995
info@anglicandar.org
actdiosm@gmail.com
habari@anglicandar.org
Ilipo Mitaa yetu
Ungana nasi kila Jumapili kwenye ibada kwa lugha ya Kiingereza kwenye baadhi ya mitaa yetu na ibada kwa lugha ya Kiswahili katika mitaa,na vigango vyetu vyote.
Pia tuna ibada za katikati ya juma, pamoja na ibada za jumuiya kila siku ya jumamosi, kwenye mitaa na vigango husika.